Karibu

Kupika kwangu ni starehe.. Napenda sana kupika! Karibu tuchangie mapishi mapya.

Tuesday, March 23, 2010

Kifungua Kinywa Mkate wa kupaka Mayai : French Toast


Imepita takriban mwaka na nusu sasa, tangu nianzishe blog hii.. nilitaka kupost lakini mambo yakawa mengi sana. Ila kwa sasa nimerudi na tutaendea kushare mambo mazuri..

Leo hii tutaona kuhusiana na kifungua kinywa (Break fast) cha Mkate wa kupaka mayai..

Aina hii ya chakula ni maarufu sana nchi za magharibi ila kwa mara ya kwanza nimekula chakula hiki nyumbani, mama yangu alipenda sana kumpkia baba..



Mahitaji


  1. Mkate vipande vinne (uliokatwa vipande vikubwa ili usilowe sana)
  2. Mayai 4
  3. Maziwa nusu kikombe
  4. Mdalasini (ama vanila) kijiko kimoja
  5. Asali vijiko viwili ama Jam ya ladha yeyote unayopenda
  6. Mafuta ya alizeti ama mafuta mazito kama kimbo.
Jinsi ya kuandaa

  1. Changanya mayai, Maziwa, Mdalasini (ama vanila).Koroga mpka uone iko tayari.(unaweza kusaga kwa blender ama kupiga kawaida tu kwa mkono).
  2. Chukua mikate yako iliyokatwa vipande vikubwa chovya kwenye mchanganyiko huo, gueza mkate halafu weka pemben kwa dakika 10 tu.
  3. Chukua kikaango weka mafuta yaive kisha anza kukaanga mikate, panga mikate itoshe kwenye kikaango. hakikisha unagueza mikate inapokuwa ya hudhurungi(brown). Kuwa makini isiungue.
  4. Chakula chako kipo tayari.. Panga kwenye sahani yako... mimina Asali kwa juu kisha pamba kwa vipande vya matunda upendayo.(ili iwe laini na nzuri ipashe asali yako kwenye microwave ama kwenye jiko lako)
  5. Chakula hiki ni kwa ajili ya watu wawili tu. 


Kila na heri na mapishi haya.. Enjoy!!

Saturday, June 14, 2008

Mapishi


Karibuni katika Blog yetu ya mapishi.. Kila wiki tutakuwa tunajifunza mapishi mapya..
Blog hii ni mahususi kwa wale wapendao kupika na wanaotaka kujifunza kupika..
Kina kaka na kina dada wote mnakaribishwa sana..
Stay tuned kwa mapishi mbali mbali.........